Tuesday, September 30, 2014

 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo.
 Makamu wa Rais IMTUSO, Walter Nnko.
Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson Lukwambe.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma kufuatia maagizo ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) dhidi ya chuo cha IMTU. Kulia ni Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson Lukwambe na Makamu wa Rais, Walter Nnko.
 
Dotto Mwaibale
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU wameiomba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuunda tume maalumu itakayoshirikisha uongozi wa wanafunzi kufuatia utekelezaji wa maagizo waliyokiwekea chuo hicho ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho,IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo alisema wanafunzi wa chuo hicho wana wasiwasi kuhusiana na muda wa miezi mitatu uliotolewa na  TCU kuhakikisha chuo cha IMTU kimekamilisha masharti yote waliyopewa vinginevyo kitafungwa.
 
"Matatizo ya chuo hicho ni ya muda mrefu hivyo kukiwa na kamati maalumu itasaidia kushughulikia suala hilo haraka na kulitafutia ufumbuzi badala ya kukifunga chuo hicho ambako kutaleta athari kubwa katika masomo kwa wanafunzi" alisema Mambo.
 
Mambo alisema TCU iunde kamati ya muda itakayoshirikiana na uongozi wa chuo uliopo sasa pamoja na uongozi wa wanafunzi waweze kusimamia na kuhakikisha kuwa maagizo ya TCU yanatekelezwa ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuendelea na masomo huku mapungufu ya muda mrefu yaliyopo yakiendelea kutatuliwa kwani muda huo wa miezi mitatu waliopewa ni mdogo.
 
Aliongeza kuwa endapo uongozi wa chuo utashindwa kutekeleza maagizo ya TCU hawaungi mkono hoja ya kufunga chuo badala yake kiwekwe chini ya serikali au chuo kikuu kingine ambacho kina kitakuwa na uwezo wa kusimamia mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaa ambacho hakina kitivo cha afya.
 
Makamu wa Rais wa Serikali ya chuo hicho, WalterNnko alisema kukifunga chuo hicho kutawaathiri wanafunzi zaidi ya 1000 waliopo chuoni hapo
filed under:

Monday, September 29, 2014

Ooh…nooo! Wachumba wa muda mrefu, staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na Malick Bandawe ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na msuguano wa chini kwa chini, hatimaye wameachana, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda mzima.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini na cha uhakika kimemwaga data kwamba wachumba hao ambao walivalishana pete kwa mbwembwe miaka mitatu iliyopita huku wakipika na kupakua lakini wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kifamilia, ambapo mara kadhaa wameripotiwa kuchapana wameachana.
“Unajua hawa jamaa wamekuwa na maisha ya kutoaminiana sana, nadhani wivu ndiyo sababu kubwa, lakini naona safari hii hali imekuwa mbaya zaidi kwa sababu Rose  ameamua kubeba kilicho chake na kuondoka kwa mwenzake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Hiyo ndiyo habari ya mjini, bidada karudi kwao (Kigogo, Dar) na mwanaye. Ilikuwa ni lazima ndoa isiwepo kwani licha ya kupata mtoto hakukuwa na furaha hata kidogo.”
TATIZO NI NINI?
Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuingia kwa undani kuhusu tatizo hasa lililotokea safari hii, lakini kilibainisha kwamba kabla ya tukio la sasa, mzozo mwingine mkubwa uliibuka kati yao.
“Kuna kipindi hali ilikuwa tete sana, Malick akaamua kuchukua mabegi yake na kutokomea kusikojulikana ambako alikaa kwa muda wa kama wiki mbili.
“Haikujulikana alikuwa wapi kwa muda wote huo, lakini baadaye tukamuona jamaa anarudi na maisha yao yakaendelea.
NDOTO YA NDOA YAYEYUKA
“Lakini wakati bado mambo hayajatulia, kumeibuka tatizo lingine kubwa ambalo limesababisha Rose kuamua kuondoka huku ndoto ya ndoa ikiyeyuka,” kilisema chanzo hicho.
VIPI KUHUSU MTOTO?
Katika mtafaruku huo, Malick alikataa katakata mtoto wake kuondoka na mama yake, lakini kutokana na umri wa mwaka mmoja wa kijana wao huyo, Naveen, alilazimika kuondoka na mama yake kwa vile bado ananyonya.
Rose Ndauka wakati akiwa na mpenzi wake, Malick Bandawe
Rose, mmoja kati ya waigizaji warembo wa filamu Bongo, inasemekana kwamba yupo nyumbani kwa wazazi wake, Kigogo kutoka kwa mchumba wake, anayeishi Tandale, Tanesco jijini Dar.
IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni ambapo stepu ya kwanza ilikuwa ni nyumbani walikokuwa wakiishi wapenzi ambapo hawakuwepo.
JIRANI ANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili juu ya kuondoka kwa Rose nyumbani hapo, mmoja wa majirani zake aliyejitambulisha kwa jina moja la Sudi alikuwa na haya ya kusema:
“Rose Ndauka ana muda hatumuoni kama miezi sasa lakini ‘mista’ tunamuonaona labda kama amehama ‘but’ sina uhakika sana.”
ROSE VIPI?
Katika kutafuta ukweli alitafutwa Rose kila kona baada ya simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani lakini jitihada ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.
BOFYA HAPA KUMSIKIA MALICK
Mchumba mtu, Malick alipoulizwa juu ya ukweli wa sakata hilo, alikiri kutokea na kwamba baada ya jitihada zake nyingi za kulinusuru penzi lao kushindikana, amekubali matokeo.
“Nimejitahidi sana kumwelewesha Rose ili apate kunielewa, ajue namna ya maisha yalivyo, lakini imekuwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu. Nimekubali yaishe.
“Kinachonisikitisha sana ni kuona kuwa mwanangu anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine, inauma sana tena sana,” alisema bila kufafanua maana ya kauli hiyo.
Katika uchumba wao mrefu, Rose na Malick wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naveen.

Sunday, November 3, 2013

Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.

Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .

Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.

Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.

Mbali ya kushuhudia shehena ya pembe hizo, alionyeshwa gari maalumu aina ya Toyota Noah ambalo watuhumiwa hao hulitumia kutoa pembe porini na kuyaingiza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika eneo la tukio mara baada ya kuwakamata alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imesitishwa na Serikali juzi baada ya wabunge kuilalamikia.

Waziri Kagasheki alisema kwamba katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa hao walitoa Sh30 milioni kwa ajili ya kujaribu kuwahonga askari.

“Walitaka kuwahonga askari ili wasikamatwe,” alisema huku akionyesha noti za fedha hizo.

Alisema wabunge wanaomtaka ajiuzulu kwa madai kwamba Operesheni Tokomeza Ujangili imesababisha mauaji ya watu na mifugo wanapoteza muda kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumtoa ni Rais Jakaya Kikwete pekee.

“Sasa mimi nasema kunitoa haitakuwa rahisi anayeweza kunitoa ni yule aliyeniweka,” alisema.

Alisema ipo mikakati inayofanywa na baadhi ya wabunge kutaka kuwang’oa baadhi ya mawaziri kwa masilahi binafsi ya kisiasa.
Itakuwa ni jambo la ajabu kwamba kila mtu akiingia madarakani wanataka atoke, watatolewa wangapi?” alihoji na kuongeza kuwa operesheni hiyo ni muhimu kwa ajili ya kunusuru tembo wasiishe.

Alisema kwamba ni kweli kuna baadhi ya dosari zimejitokeza kwenye operesheni ikiwamo kuuawa kwa baadhi ya mifugo, lakini siyo kwamba zoezi zima halina manufaa.

Kagasheki alisema kama kasi hii ya kuuawa kwa tembo itaachiwa iendelee baada ya miaka 10 tembo wote watakuwa wameisha nchini.

Alisema hataki kuona utawala wa Rais Kikwete ukiondoka madarakani ukiwa na lawama ya kuachia majangili wawamalize tembo.

Mmoja wa watuhumiwa hao, Huang Qin alisema shehena yote ya pembe za ndovu iliyokamatwa nyumbani kwake ilikuwa ikiletwa kidogo kidogo na rafiki yake ambaye hakumtaja jina.

Akiongea kwa Kiswahili Qin alisema: “Mimi hii si yangu, kichwa yangu mbovu. Rafiki yangu alileta hii (pembe) kidogo kidogo.”

Januari mwaka huu, Gazeti La Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba Serikali ya Kenya imekamata shehena ya vipande 638 vya pembe za ndovu ambavyo ni sawa tembo 320 waliouawa.

Mzigo huo wa tani mbili ulikuwa kwenye kontena la mawe ya urembo (marumaru) kutoka Tanzania.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa tani nne za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 3.4 milioni sawa na takriban Sh5.4 bilioni zilikamatwa Hong Kong Oktoba 20, mwaka jana, huku ikielezwa kuwa meno hayo yalikamatwa yakisafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.

Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na pembe za ndovu yenye thamani ya Sh18.4 milioni yaliyotengenezwa kama bangili tayari kusafirisha kwenda nje ya nchi.
Mwananchi
filed under:

Monday, September 16, 2013


Kesi inayomkabili waziri mkuu Mizengo  Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali  imetajwa mahakamnai kwa mara ya  kwanza ambapo  wamewasilisha pingamizi  la  awali dhidi ya  kesi ya kikatiba waliyofunguliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu  kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika.
   
Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS,wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kutokana na kauli  aliyoitoa bungeni hivi karibuni  wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria kuwapiga wananchi  wakati wa vurugu. 
 
 
Hata hivyo Pinda na  mwanasheria mkuu  kwa pamoja katika majibu yao ya madai hayo, wamewasilisha pingamizi la awali ambapo  pamoja na mambo mengine wamedai   kuwa walalamikaji na watu  walioorosheshwa katika kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.
 
 
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la  majaji watatu likiongozwa na jaji kiongozi, Fakihi Jundu akisaidiana na jaji Dk Fauz Twaib na jaji Augustine Mwarija ambapo  upande wa wadaiwa uliwakilishwa na mawakili wa serikali wakuu watatu, Nickson Mtingwa, Sarah Mlipana na Alesia Mbuya.
 
 
Aidha  upande wa walalamikaji uliwakilishwa na mawakili wanne kati ya saba waliotajwa  awali .Akizungumza na waandishi  wa habari nje ya mahakama hiyo,  mmoja ya mawakili hao amesema  wamepewa siku  14 kujibu pingamizi lililotolewa .
 
 
Wakati kesi hiyo ilipotajwa mahamani hapo  upande wa madai uliomba siku 21 kuwasilisha  majibu ya wadaiwa ambapo hata hivyo wakili wa serikali mkuu, Mtingwa, alipinga ombi hilo katika kipengele cha muda ulioombwa na badala yake  akapendekeza wapewe siku 14 tu.
 
 
Mahakama katika uamuzi wake uliosomwa na jaji kiongozi Jundu, ilikataa ombi la wadai na kukubaliana na ombi la wadaiwa, na kuwapa wadai siku 14 badala ya siku 21 kama walalamikaji walivyomba ili kuweza kuwasilisha majibu yao.
 
 
Mahakama hiyo iliamuru wadai wawasilishe mahakamani majibu yao  kabla au septemba 30, na kupanga kusikiliza pingamizi la awali la wadaiwa oktoba 18.
 
Itakumbukwa kuwa pinda alitoa kauli hiyo inayolalamikiwa, katika mkutano wa 11 wa bunge wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu bungeni, juni 20,2013
filed under: ,

 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshtaki Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youging kwa Umoja wa Mataifa (UN) kwa kujihusisha na siasa katika majukwaa nchini kitendo ambacho ni hatari katika uhusiano wa diplomasia kati ya Tanzania na China.

Pia kimemshtaki kwa Serikali ya China na ya Tanzania kikidai kitendo cha balozi huyo ni kukiuka Mkataba wa Kidiplomasia wa Vienna (Vienna Convention of Diplomatic Reletions of 1964 ibara ya 41 (1-3) ambao unasimamia sheria za nchi wanachama w Umoja wa Mataifa. 


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chadema, Ezekiel Wenje alisema kitendo cha Balozi wa China, Dk. Youging kujihusisha na siasa za uenezi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kosa kubwa kimataifa na amepoteza sifa za kushikilia nafasi hiyo.

Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema balozi huyo amevunja sheria za Mkataba wa Vienna ambao unasimamia sheria za nchi wanachama wa UN.

Alisema kifungu alichovunja kinakataza Balozi yeyote kujihusisha na shughuli nyingine ambazo haziendani na majukumu ya uwakilishi wa nchi na nchi.

Wenje alisema balozi huyo anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kama inavyoelekezwa katika mkataba wa Vienna kwamba ikiwa balozi atakiuka mkataba huo atakosa sifa na ataondolewa kinga aliyonayo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema: “Jambo hili katika macho ya diplomasia, limevunja misingi na taratibu za ushirikiano wa kimataifa, wenye nia njema kwa wananchi wa pande mbili, baina ya nchi na nchi na katika ngazi ya serikali.

“Kwanza ni taswira ya dharau ya hali ya juu ambayo Balozi wa China ameamua kuwaonyesha Watanzania, hatuamini kwamba amepungukiwa na uwezo kiasi gani lakini anapaswa kukumbushwa aweze kuheshimu mipaka ya majukumu na wajibu wa diplomasia kwa nafsi ya balozi anapokuwa nchi ya ugenini.

“Balozi huyu anapaswa kukumbushwa kuwa uhusiano wa vyama, kwa maana ya Chama cha Kikomunisti cha China na CCM hata kama ungekuwa mzuri kiasi gani hauna mwingiliano na uhusiano wa Serikali ya Tanznaia na China.

“Hatutaki kuamini kuwa serikali ya China imemtuma Balozi Youquing kuja nchini kufanya kazi za ukatibu mwenezi wa CCM, tumesikitishwa heshima aliyopewa na Watu wa China ameidharau na amevuka mstari ambao hakuna mwanadiplomasia yeyote makini anayeheshimu uhusiano baina ya nchi na nchi angejaribu kufanya hivyo.

“Mstari aliouvuka balozi huyu umefafanuliwa wazi katika Mkataba wa Vienna Convention wa 1961 hasa katika kifungu cha 41(1) na 3, katika masuala yanayohusu uhusiano na kinga za mabalozi, kwamba ni marufuku kwa mwanadiplomasia yeyote kuingilia siasa za ndani za nchi mwenyeji wake.

“Chadema tunachukua hatua dhidi ya balozi huyo kujihusisha na chama cha siasa kwa kuvaa kofia ya CCM na kuelezea mambo ambayo hayakupaswa kusemwa kwenye majukwaa ya siasa.

“Kwanza tunaandika barua tatu, moja itakwenda Serikali ya China, ya pili itakwenda UN na nyingine itakwenda Serikali ya CCM ambayo ndiyo imempeleka huko mikoani.

“Barua hizo zitakuwa zinataka kueleza msimamo wa tukio hilo la balozi wa China nchini kujihusisha na siasa za majukwaani na kuvaa nguo za CCM, tunataka kujua hatua gani zitakazochukuliwa haraka kabla ya Chadema hatujapendekeza hatua za kuchukua.

“Hii ni hatari kwa balozi huyo kujiingiza kwenye siasa kitendo kinachosababisha kuhatarisha uhusiano uliopo kati ya wawekezaji wa China nchini kwa sababu wananchi wanaweza kutafsiri vibaya.

“Kwa mfano kuna maeneo ni ngome za Chadema na pale kuna wawekezaji wa China wanaweza kukataa kutoa ushirikiano wakidai ni wapo mlengwa wa CCM, pia ni hatari chama kingine kitapokuja kushika dola hakutakuwa na uhusiano mzuri.

“Tutaambatanisha ushahidi wa kutosha katika barua hizo ikiwa ni pamoja na picha za mnato na video, maneno aliyotamka kwenye mkutano, picha inayoonyesha akiwa amveaa sare za CCM na jinsi anavyocheza”.

Picha zilizonyeshwa kwa waandishi wa habari zilionyesha Balozi Youging akiwa katika mikutano mbalimbali ya CCM maeneo ya Kishapu, Shinyanga na Kahama.

Katika picha hizo balozi huyo alionekana amevaa sare za CCM, akihutubia na kuendesha baiskeli akiwa na viongozi wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Kwa mara ya kwanza balozi huyo aliibukia katika mkutano waCCM uliofanyika Shinyanga huku akishangiliwa na wananchi alipojaribu kuzungumza kisukuma.


CCM yazungumza
Wakati huohuo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumshutumu Balozi wa China, Dk. . Lu Youqing kwa kuhudhuria mikutano ya CCM.

Kimewataka watanzania kupuuza madai ya Chadema kikisema hayana msingi kwa maendeleo ya taifa na watu wake.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.

Alisema ni wazi Chadema kinataka kutumia matatizo ya wananchi kuyageuza agenda ya siasa.

Chadema haina budi itambue kuwa chama tawala cha China (CPC) kimekuwa na urafiki wa muda mrefu na CCM ikizingatia Balozi Dk. Lu pia ni kiongozi wa chama hicho.

Nape alisema hatua ya Balozi huyo kuhudhuria mkutano huo ni mafanikio ya ziara ya iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana China mapema mwaka huu.

“Balozi Dk. Lu amekuja kuleta ukombozi kwa watanzania hasa wa Kanda ya Ziwa kwa kuleta wawekezaji katika Mkoa wa Shinyanga kwa kujenga viwanda wa nyuzi, pamba, nyama, maji na ngozi ambako ajira zaidi ya 1000 zitapatikana.

“Watanzania wapuuze madai haya kwani si dhambi kwa Balozi wa China kuhudhuria mkutano wa CCM… urafiki wetu hakuanza leo ni wa muda mrefu katika historia ya nchi hizi mbili tangu na baada ya Uhuru,” alisema Nape.

Nape alisema CCM imepitaka kila eneo la yakiwamo majimbo yanayoongozwa na wapinzani na kubaini kuwapo changamoto nyingi.

Aliitaka Chadema kwenda kutatua haraka matatizo hayo badala ya kufanya mikutano Dar es Salaam pekee.

Wiki iliyopita akiwa mjini Shinyanga Balozi Dk. Lu Youqing, alihudhuria mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa hakuna chama imara kama hicho
filed under: ,


Hivi sasa producer wa wimbo wa" kaka dada" ameamua kumvisha pete mpenzi wake ambaye amekuwa mchumba wake rasmi.

Akiongea na millardayo,Lucci  alikuwa  na  haya  ya  kusema: “Baada ya mambo ya project ya Kaka Dada kukamilika nimeona ni muda muafaka kabisa kumvisha pete mpenzi wangu Lisa Semgeliwa au marafiki zake huwa wanamuita Lizzyblazzer. 

"Unajua like seriously tumekuwa kwenye dating kwa muda zaidi ya miaka 2. Muda huo unatosha kabisa naamini ni vizuri kuingia kwenye hatua nyingine ya mahusiano yetu” .
 
Wengi  wanajiuliza, huyu shemeji yetu alikuwa na hali gani kipindi kifupi kilichopita wakati "Kaka Dada"  ikiwa  JIKONI  na  baada  ya  kutoka????...

Lucci  analitolea  ufafanuzi  jambo  hilo:
”Unajua ukishakuwa kwenye mapenzi na mtu anayejitambua na anaefahamu kazi yako. Basi atafahamu kabisa entertainment inahitaji vitu tofauti ili kufanikisha. 

"So mimi na yeye tuliongea kwamba muda huu tunaitoa kazi ya kaka dada na plan nzima alikuwa anaijua. So hakukuwa na tatizo lolote”
 
Baada  ya  maelezo  hayo,Lucci  aliamua  kuelezea   kuhusu mchumba wake:

”Lisa ni director wa kampuni yetu mimi na yeye inaitwa  Tsere. Kazi tunayofanya ni creative and marketing, pia anafanya kazi ya HR kwenye hii kampuni”

Ni  imani  yangu  kuwa  Lucci  ameamua  kufunguka  ili  kuzima  tuhuma  zilizokuwa  zikisambaa  kwa  kasi  kuhusu  kutoka  kimapenzi  na  Jokate. 
filed under: ,
PICHA za mwigizaji Flora Mvungi (Hadija) ambaye ni mke wa msanii Hamis Baba ‘H. Baba’ akijifungua mtoto wa kike baada ya kusota kwa muda mrefu ZIMEVUJA
 Flora Mvungi (Hadija) akijifungua.
Kutoka kwa vyanzo vyake, mbali na picha za mtoto, Mwandishi wetu alilibamba tukio la Flora akijifungua Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes iliyopo Sinza, Dar.

Flora akiwa hospitali na mumewe H. Baba.
Kwa mujibu wa H. Baba, alifurahishwa kuitwa baba kwani ni kitu ambacho alikuwa anatamani kwa muda mrefu na Mungu amemtimizia hivyo anamshukuru kwani ni zawadi kubwa katika maisha yake.

Mtoto wa Flora Mvungi.
Kwa upande wa Flora alikuwa na haya ya kusema: “Namshukuru sana Mungu kwa sababu niko salama na mwanangu, ukweli mwacheni mama aitwe mama kwani kuzaa siyo kazi rahisi”.
 
H. Baba alimalizia kwa kusema kuwa kama walivyosema awali kabla mtoto huyo hajazaliwa kuwa jina lake ataitwa Tanzanite, ndiyo hivyo itakavyokuwa jina hilo ndilo litakalotumika.
filed under: ,
Copyright © 2013 LEO HABARI BLOG | Powered by Blogger