Tuesday, September 30, 2014

 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo.
 Makamu wa Rais IMTUSO, Walter Nnko.
Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson Lukwambe.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma kufuatia maagizo ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) dhidi ya chuo cha IMTU. Kulia ni Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson Lukwambe na Makamu wa Rais, Walter Nnko.
 
Dotto Mwaibale
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU wameiomba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuunda tume maalumu itakayoshirikisha uongozi wa wanafunzi kufuatia utekelezaji wa maagizo waliyokiwekea chuo hicho ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho,IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo alisema wanafunzi wa chuo hicho wana wasiwasi kuhusiana na muda wa miezi mitatu uliotolewa na  TCU kuhakikisha chuo cha IMTU kimekamilisha masharti yote waliyopewa vinginevyo kitafungwa.
 
"Matatizo ya chuo hicho ni ya muda mrefu hivyo kukiwa na kamati maalumu itasaidia kushughulikia suala hilo haraka na kulitafutia ufumbuzi badala ya kukifunga chuo hicho ambako kutaleta athari kubwa katika masomo kwa wanafunzi" alisema Mambo.
 
Mambo alisema TCU iunde kamati ya muda itakayoshirikiana na uongozi wa chuo uliopo sasa pamoja na uongozi wa wanafunzi waweze kusimamia na kuhakikisha kuwa maagizo ya TCU yanatekelezwa ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuendelea na masomo huku mapungufu ya muda mrefu yaliyopo yakiendelea kutatuliwa kwani muda huo wa miezi mitatu waliopewa ni mdogo.
 
Aliongeza kuwa endapo uongozi wa chuo utashindwa kutekeleza maagizo ya TCU hawaungi mkono hoja ya kufunga chuo badala yake kiwekwe chini ya serikali au chuo kikuu kingine ambacho kina kitakuwa na uwezo wa kusimamia mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaa ambacho hakina kitivo cha afya.
 
Makamu wa Rais wa Serikali ya chuo hicho, WalterNnko alisema kukifunga chuo hicho kutawaathiri wanafunzi zaidi ya 1000 waliopo chuoni hapo
filed under:

Monday, September 29, 2014

Ooh…nooo! Wachumba wa muda mrefu, staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na Malick Bandawe ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na msuguano wa chini kwa chini, hatimaye wameachana, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda mzima.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini na cha uhakika kimemwaga data kwamba wachumba hao ambao walivalishana pete kwa mbwembwe miaka mitatu iliyopita huku wakipika na kupakua lakini wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kifamilia, ambapo mara kadhaa wameripotiwa kuchapana wameachana.
“Unajua hawa jamaa wamekuwa na maisha ya kutoaminiana sana, nadhani wivu ndiyo sababu kubwa, lakini naona safari hii hali imekuwa mbaya zaidi kwa sababu Rose  ameamua kubeba kilicho chake na kuondoka kwa mwenzake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Hiyo ndiyo habari ya mjini, bidada karudi kwao (Kigogo, Dar) na mwanaye. Ilikuwa ni lazima ndoa isiwepo kwani licha ya kupata mtoto hakukuwa na furaha hata kidogo.”
TATIZO NI NINI?
Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuingia kwa undani kuhusu tatizo hasa lililotokea safari hii, lakini kilibainisha kwamba kabla ya tukio la sasa, mzozo mwingine mkubwa uliibuka kati yao.
“Kuna kipindi hali ilikuwa tete sana, Malick akaamua kuchukua mabegi yake na kutokomea kusikojulikana ambako alikaa kwa muda wa kama wiki mbili.
“Haikujulikana alikuwa wapi kwa muda wote huo, lakini baadaye tukamuona jamaa anarudi na maisha yao yakaendelea.
NDOTO YA NDOA YAYEYUKA
“Lakini wakati bado mambo hayajatulia, kumeibuka tatizo lingine kubwa ambalo limesababisha Rose kuamua kuondoka huku ndoto ya ndoa ikiyeyuka,” kilisema chanzo hicho.
VIPI KUHUSU MTOTO?
Katika mtafaruku huo, Malick alikataa katakata mtoto wake kuondoka na mama yake, lakini kutokana na umri wa mwaka mmoja wa kijana wao huyo, Naveen, alilazimika kuondoka na mama yake kwa vile bado ananyonya.
Rose Ndauka wakati akiwa na mpenzi wake, Malick Bandawe
Rose, mmoja kati ya waigizaji warembo wa filamu Bongo, inasemekana kwamba yupo nyumbani kwa wazazi wake, Kigogo kutoka kwa mchumba wake, anayeishi Tandale, Tanesco jijini Dar.
IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni ambapo stepu ya kwanza ilikuwa ni nyumbani walikokuwa wakiishi wapenzi ambapo hawakuwepo.
JIRANI ANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili juu ya kuondoka kwa Rose nyumbani hapo, mmoja wa majirani zake aliyejitambulisha kwa jina moja la Sudi alikuwa na haya ya kusema:
“Rose Ndauka ana muda hatumuoni kama miezi sasa lakini ‘mista’ tunamuonaona labda kama amehama ‘but’ sina uhakika sana.”
ROSE VIPI?
Katika kutafuta ukweli alitafutwa Rose kila kona baada ya simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani lakini jitihada ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.
BOFYA HAPA KUMSIKIA MALICK
Mchumba mtu, Malick alipoulizwa juu ya ukweli wa sakata hilo, alikiri kutokea na kwamba baada ya jitihada zake nyingi za kulinusuru penzi lao kushindikana, amekubali matokeo.
“Nimejitahidi sana kumwelewesha Rose ili apate kunielewa, ajue namna ya maisha yalivyo, lakini imekuwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu. Nimekubali yaishe.
“Kinachonisikitisha sana ni kuona kuwa mwanangu anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine, inauma sana tena sana,” alisema bila kufafanua maana ya kauli hiyo.
Katika uchumba wao mrefu, Rose na Malick wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naveen.
Copyright © 2013 LEO HABARI BLOG | Powered by Blogger